Na Shomari Binda,Musoma
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Bibi Majira mkazi wa Kata ya
Nyakato katika Manispaa ya Musoma ameuwawa na Wananchi wenye hasira kali
kutokana na kutuhumiwa kushiriki katika Vitendo vya kishirikina.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii jioni ya leo mara baada ya
Tukio hilo lililotokea Mchana katika Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya
hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi
Absalom Mwakyoma amesema Mwanamke huyo alifariki Dunia mara baada ya
kufikishwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mara baada ya kupata Jeraha kubwa
la panga katika upande wa kushuto wa Kichwa chake.
Kamanda Mwakyoma amesema Mwanamke huyo alivuja Damu nyingi baada ya
kushambuliwa na Wananchi hao na hali yake ilikuwa mbaya zaidi mara baada
ya kufikishwa katika Hospitali hiyo na alifariki baada ya muda mfupi.
Amesema si vyema kujichukulia sheria mikononi na kupoteza Uhai wa
Binadamu kwa Imani za kishirikina na kusema Kitendo hicho ni kinyume cha
Haki za Binadamu ambacho kinaweza kuleta Matatizo katika Jamii.
Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara amesema ajakipenda
kitendo hicho na kukilani na kuitaka Jamii kubadilika na kujiepusha
navyo kwani kunaweza kumuingiza Mhusika wa Matukio hayo katika Matatizo
asiyoyategemea.
Amesema Jeshi la Polisi litaendelea kufatilia na litamfikisha katika
Vyombo vya Sheria Mwananchi yeyote atakayebainika kuhusika katika tukio
hilo ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Awali wakizungumza na Mwandishi wa Habari hii katika eneo la tukio
hilo,Wananchi hao wa Kata ya Nyakato walisema wameamua kuchukua Sheria
mkononi kutokana na kudai kuwepo kwa Matukio ya kishirikina katika Kata
hiyo huku Serikali ikisema haitambui Imani za kichawi.
No comments:
Post a Comment