Na Deogratius Temba
WAANDISHI wa habari wameaswa kubeba sauti za wananchi
walioko pembezoni katika kudai haki zao hasa wakati wa mchakato wa
kukusanya maoni ya wananchi kwaajili ya kuandaa katiba mpya.
Akizungumza Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia
kilichoko chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Dorothy Mbilinyi,
amesema watanzanzia masikini walioko pembezoni wanategemea kupata taarifa na
kutoa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
“ Wananchi wameamka wameanza kujieleza vyombo
vya habari vinatakiwa kufanya kazi yake kuwa sauti ya wanyonge, viwe mdomo kwa
makundi yaliyowekwa pembezoni, ili kuibua changamoto zilizojificha na kuyafanya
makundi haya kuwa na haki sawa na wengine,” amesema Mbilinyi.
Mbilinyi amesema kuwa vyombo vya habari vya Tanzania
vimefanya kazi kubwa ya kuibua kero za wananchi na ufisadi, ikiwepo kudai
uwajibikaji katika misingi ya demokrasia na haki za biandamu.
Aidha amewataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa
bidii mwaka huu kwasababu ni mwaka wenye changamoto nyingi ambazo
zitahitaji weledi, uadilifu, ukweli na uwazi.” Huu nini mwaka wa
kukusanya maoni ya katiba, mwaka wa kudai uwajibikaji kwa viongozi wasio
waadilifu, na ni mwaka wa Sensa ya idadi ya watu…” amesema Mbilinyi.
Akieleza malengo ya mafunzo hayo ya siku tatu yaliyoanza mei
3 hadi 5, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na habari, Lilian Liundi amesema kuwa
mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kujitadhimini upya jinsi ambavyo wanaandika
habari za kijinsia.
Pamoja na kujitadhimini waandishi wa habari watajifunza juu
ya hali ya sasa ya ujenzi wa vuguvugu la ukombozi wa wanawake
kimapinduzi, kampeni ya haki uchumi, mfumo dume na mfumo uleberali mambo
leo.
Pia watajifunza namna ya kuandika habari za kijinsia na
kuchambua maoni yanayotolewa na wananchi juu ya katiba mpya, kufanya
habari za kiuchunguzi vijijini na kuibua changamoto za wananchi.
Mafunzo haya yanafanyika ikiwa ni siku chache baada ya TGNP
kukutana na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es alaam wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment