Wednesday, September 8, 2010
DR. SLAA AFUNGULIWA MASHTAKA MAHAKAMA KUU
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa (pichani), amefunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaami, akidaiwa fidia y ash. bilioni moja kwa madai ya kunyang’anya mke wa mtu.
Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa jana mahakamani hapo na Aminiel Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.
Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang’anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.
Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo, kumtangaza mkewe wa ndoa Josephine kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.
Mlalamikaji huyo, anadai Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Baruti, Dar es Salaam.
Pia anadai katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.
Mahimbo alidai, ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake halali.
Kwa mujibu wa hati hiyo, Mahimbo alidai hivi karibuni, mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi. Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.
Alidai katika tarehe na mahali tofauti, Dk. Slaa alimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, suala ambalo si kweli.
Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha kimahusiano na mkewe.
Anaiomba mahakama kumwamuru Dk. Slaa kumlipa bilioni moja na kulipa gharama za kuendeshea kesi.
Mahimbo amedai ameambatanisha na cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
MIMI SUALA LA KUCHUKUA MKE WATU NISINGEPENDA KULIZUNGUMZIA MAANA BADO LIKO MAHAKAMANI. LA MHIMU KWANGU NI KWAMBA DR SLAA NA CHAMA CHAKE BADO HAJAWA NA UWEZO WA KUCHUKUA DOLA. CHAMA CHAKE BADO NI CHA KIKANDA. NDIO MAANA KIMESHINDWA KUPATA HATA ASILIMIA 4 YA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA. KIMISHINDWA HATA KUSIMAMISHA ASILIMIA 30 YA WAGOMBEA UDIWANI NCHINI. KIMESHINDWA KUSIMAMISHA HATA ASILIMIA 40 YA WOGOMBEA UBUNGE. HIYO KATIBA MPYA YA SIKU MIA ITAPITISHWA NA BUNGE LIPI? HIYO ELIMU YAKE YA BURE ITATOLEWA NA FEDHA ZILIZOPITISHWA NA BUNGE LIPI?
UWEZO WA DR SLAA UNGEONEKANA KWANZA KATIKA CHAMA. MUDA WA MIAKA KUMI NA SABA YA UHAI WA CHADEMA NI MUDA MREFU SANA. KWA CHAMA MAKINI CHENYE VIONGOZI MAKINI KINGEKUWA KIMESHASAMBAA NCHI NZIMA. CHADEMA KWA SASA BADO HATA HAWANA OFISI INAYOWEZA KUITWA OFISI YA KITAIFA YA CHAMA KINACHOTAKA KWENDA IKULU. MIKOANI NI SEHEMU CHACHE SANA AMBAKO WANA OFISI. SEHEMU NYINGI TUNAWAONA VIONGOZI NA MAFAILI YAO KATIKA MAGARI YENYE VIBAZA SAUTI.
UBORA WA URAISI HAUPIMWI KWA KUKOSOA UTAWALA ULIOPO TU. KUKOSOA NI KITU RAISI SANA. KAMA INGEKUWA KUKOSOA NDIO KIPIMO CHA URAISI MTIKILA ANGEKWISHAKUWA RAISI MUDA MREFU.
MWALIMU NYERERE AMBAYE DR SLAA ANAJARIBU KUJIFANANISHA NAO ALIPIMWA KWANZA KWA UWEZO WA KUKIIUZA CHAMA NCHI NZIMA. CHAMA KILIENEA KILA KONA YA NCHI NA HATIMAYE KIKAWEZA KUSHIKA DOLA.
CHADEMA WANGEKUWA MAKINI WASINGETUMIA KARIBU FEDHA ZOTE KUKODISHA NDEGE YA KAMPENI KWA MGOMBEA URAISI HUKU WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI WAKIWA KAPA.
Post a Comment