Na Pendo Omary , Tarime.
Tamasha la Jinsia Limefunguliwa katika kijiji cha
Ng’ereng’ere, kata ya Nyamaraga Tarime.
Mada kuu ikiwa “ Ukeketaji, Ndoa za utotoni na Haki ya uchumi”.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa tamasha hilo, Kaimu
mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mary Nsemwa amesema, tamasha
hilo ni fursa ya kuwakutanisha viongozi, wanaharakati na wananchi katika
kutafakari changamoto, fursa na namna ya kuchukua hatua katika kukomesha ukatili wanaofanyiwa wanawake na watoto wa
kike kwa kuzingatia muktadha.
“Tamasha la jinsia ni jukwaa la wazi, linalowaleta pamoja
watu, tasisi na viongozi kukutana na kupashana habari, kutafakari na
kusheherekea harakati hasa kwa kuangalia
muktdha.” Amesema Nsemwa.
Aidha mtoa mada katika tamasha hilo, mwazilishi wa shirika
la Kivulini , Maimuna Kanyamala amesema, wameamua kuongelea mada hiyo Tarime kwa
sababu wanajali utu wa kila mtu bila kujali umri, elimu, dini, kabila na
itikadi, ambapo wanaotendewa ukatili huo ni watoto wa kike na wanawake ambapo ni kinyume cha
haki za binadamu.
“Tunaongelea masuala haya Tarime kutokana na hali halisi
ilivyo. Mkoa wa Mara unaongoza kwa asilimia 72 ya ukatili wa kimwili na
kijinsia. Pia Mara ni kati ya mikoa mitatu nchini Tanzania ambayo inaongoza kwa
kiwango kikubwa sana cha ndoa za utotoni,” amesema Kanyamala.
Mgeni rasmi katika Tamsha hilo, Afisa Utawala wa wilaya hiyo
Baraka Nyamsenda amesema, bado jitihada zaidi zinahitajika katika kukomesha
ukeketaji kwa watoto wa kike.
“Halimashauri ya wilaya ya Tarime inajitahidi kukomesha
ukeketaji, lakini jitihada zaidi zinahitajika kwa sababu jamii hufanya
ukeketaji kwa siri,” amesema Nyamsenda.
Tamasha
hilo limefadhiliwa na Shirika linaloshughurikia idadi ya watu duniani (UNFPA)
litafanyika kwa siku tatu ambapo washiriki zaidi ya 500 wanahudhuria kutoka
mikoa ya Mara, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam, Morogoro na Shinyanga. Washiriki wengine ni OXFAM,
No comments:
Post a Comment