Monday, July 21, 2014

Mtandao wa wanawake na katiba wataka wahariri kuandika habari za jinsia



Mtandao wa wanawake  na katiba wataka wahariri kuandika habari za jinsia

Na Deogratius Temba
MTANDAO wa wanawake na katiba umewataka wahariri wa vyombo vya habari nchini kuthamini habari za kijinsia wakati huu wa m
Mkurugenzi wa TAMWA akizunguma na wahariri

Wahariri waliofika kusikiliza ujumbe wa wanawake na katiba

Mkurugenzi akiendelea

Wahariri wakifuatilia  kwa umakini

Mjumbe wa Mtandao Dk. Avemaria Semakafu akitoa mada

wahariri wakifuatilia mjadala huo katika ofisi za tamwa Sinza.
chkato wa kuandaa katiba ili kuhakikisha masuala ya jinsia yanapewa kipaumbele katika mijadala mbalimbali na kuingizwa kwenye katiba mpya.

Akizungumza wakati wa mkutano na wahariri mbalimbali kutoka vyombo vya habari hapa nchini na vya kimataifa, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa habari wanawake (TAMWA), Valeria Musyoka mwishoni mwa wiki alisema kuwa  Mtandao wa wanawake na katiba umeweka mkakati wa kukutana na wanahabari hasa wahariri ili kujenga nguvu ya pamoja katika kuibua mijadala na kuhakikisha jamii inaelewa maanaa halisi ya dhana ya jinsia na kuipigania ili iweze kuingizwa kwenye katiba mpya.

Alisema kuwa masuala makuu ambayo asasi zinazounda umoja wa wanawake na katiba zinazoyapigania ni pamoja na haki ya kulindwa na kuthaminiwa, Kupata elimu na Haki ya kushiriki katika ngazi za maamuzi.
Aidha alisema kuwa  hayo yote hatyawezi kufikiwa kama huduma za kijamii hazitaboreshwa na kuwepo kwa mgawantyo sawa wa rasilimali ili kuyapa makundi yote hasa wanawake fursa ya kunuifaika na kufikia uasawa wa kijinsia.

Kumekua na upungufu wa mabweni kwa watoto wa kike unaochangia kuacha shule kwa sababu ya mimba” alisema

Alisema kuwa jinsi ambavyo watunga sera na jamii inavyoelewa jambo na kuamua kuchukua hatua ni kutokana na habari au taarifa wanazozipokea ambazo ndizo zitakazochochea mjadala katika jamii na
kuhamasisha kuungwa mkono au kupingwa kwa hali iliyopo pamoja na sera zilizopo.

Hivyo vyombo vya habari, kama msingi wa kupatikana kwa taarifa yoyote, na kuongoza katika ushawishi vina sehemu muhimu sana katika kuongoza kuleta mabadiliko yawe ya sera, tabia au utamaduni.

Kwa upande wake mjumbe wa Mtandao huo, Dk. Avemaria Semakafu, alisema kuwa wahariri wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanasoma kwanza rasimu ya pili waielewe na kupitia taarifa mbalimbali zaini ili kujenga uelewa juu ya kitu kinachotakiwa kwenye mchakato huu wa katiba.
Aliwaasa wahariri kuweka mkazo kwenye habari za kijamii hasa uchunguzi  wa kihabari ili kubaini channzo cha uhaba wa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali.

Mtandao wa Wanawake na Katiba ni muunganiko wa asasi za kijamii na kitaaluma zipatazo hamsini zilizoungana kudai katiba inayozingatia masuala ya kijinsia na inayotokana na mchakato ulioshirikisha sauti za makundi yote.

No comments: