Tuesday, March 27, 2012

TGNP Yapeleka Waandishi wa Uchunguzi Kisarawe

Bi. Kenny Ngomuo (kulia) akizungumza na wanaharakati wa Kata ya Manerumango

Bi. Kenny Ngomuo akitoa maelekezo kwa wanaharakati wa Maneromango

Baadhi ya wanaharakati wa Kata ya Manerumango wakiangalia moja ya ripoti zilizoandaliwa na TGNP kabla ya kuanza kwa mahojiano

Bi. Kenny Ngomuo (kulia) akisalimiana na wanaharakati wa Kata ya Manerumango alipokuwa akiwasili na baadhi ya wanahabari eneo ambalo waandishi walikutana na wanaharakati hao kabla ya kuanza kutembelea maeneo mbalimbali leo. Anayemfuatia ni Bi. Anna Sangai kutoka Kitengo cha Uhamasishaji Jamii TGNP. (Picha na joachim Mushi, Thehabari.com)


Na Joachim Mushi, Kisarawe

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo umepeleka baadhi ya waandishi wa habari za uchunguzi wilayani Kisarawe, Mkoa wa Pwani kuangalia matokeo ya utafiti walioufanya mwaka 2010 juu ya baadhi ya huduma za jamii hasa za afya na maji eneo hilo.

Akizungumza wilayani Kisarawe Ofisa Habari wa TGNP, Kenny Ngomuo alisema wameamua kupeleka baadhi ya waandishi wa habari kuangalia mrejesho wa utafiti walioufanya mwanzoni mwa mwaka 2010 kuangalia huduma mbalimbali za msingi kwa jamii.

Mwaka 2010 TGNP ilipeleka timu ya waandishi wa habari wilayani Kisarawe kufanya uchunguzi na kuibua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili wakazi wa eneo hilo.

Akitoa taarifa fupi kwa wanahabari na waandishi wa habari na wanaharakati Bi. Ngomuo alisema waandishi hao watatembelea vijiji mbalimbali ambavyo vilihusishwa katika uchunguzi wa awali na kuangalia tofauti iliyopo sasa ikiwa ni miaka takriban mitatu tangu kufanyika kwa uchunguzi wa awali.

Alisema waandishi hao watafanya mahojiano na wananchi, wanaharakati na baadhi ya viongozi wa kata zilizofanyiwa utafiti kuangalia tofauti iliyopo tangu kufanyika kwa uchunguzi wa awali, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo ya huduma za jamii katika maeneo hayo.


No comments: