Watu wanaoishi na changamoto za ulemavu wakifuatilia mjadala huo Dodoma |
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakifuatilia |
Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakisikiliza madai ya wananchi kwenye rasimu ya Katiba itakayojadiliwa Bungeni wiki hii |
Uongozi wa Bungwe Maalum la Katiba mbadala (Bunge Kivuli) wakiendelea kuongoza Bunge hilo Mjini Ddodoma, Katikati ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Dk. Visencia Shule |
kundi la wasichana kutoka mikoa mbalimbali wakiomba katiba mpya ikataze ndoa za utotoni |
WANAHARAKATI wanaoshiriki kongamano la Katiba la kujadili masuala ya kijinsia yanayotakiwa
kuzingatiwa kwenye mjadala wa Bunge maalum la Katiba wamewataka wajumbe wa
Bunge maalum la Katiba kuhakikisha katiba mpya itakayotengenezwa inatamka umri wa
kuolewa au kuoa uwe miaka 18 hadi 21 ili kuwapa nafasi watoto wa kike kupata
nafasi ya kusoma na kukua.
Wakizungumza wakati wakiendesha Bunge kivuli au Bunge maalum
maalum la Katiba lililoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirkiana na Mtandao wa
Wanawake na katiba mjini Dodoma, wanaharakati hao wamesema kuwa wajumbe wa Bunge maalum bila kujali tofauti
zao za kijinsi wanapaswa kuhakikisha wanapigania haki ya mtoto wa kike kuwa
salama na kutokuolewa kabla ya kukomaa akiwa na umri wa chini ya miaka 18.
Akizungumza Mwenyekiti wa Bunge maalum Mbadala la Katiba Dk.
Vicensia Shule amesema kuwa wananchi
wote wanatakiwa kuunganisha nguvu wakati huu wa mchakato wa Bunge la Katiba
kuhakikisha masuala muhimu ya wanawake nay ale ambayo yanatoa ulinzi kwa
makundi yaliyoko pembezoni yanazingatiwa na kuingizwa kwenye katiba mpya.
“hakuna taifa ambalo ni tajiri au watu wake wameendelea bila
kupata elimu, na kuzingatia usawa wa
kijinsia. Haya yote yatafanyika kama kuna elimu ya kutosha kwa wasichana na
kama wataolewa wakiwa watoto hawataweza
kupata elimu”alisema Dk Shule.
Mshiriki kutoka shirika la Active Youth of Tanzania Mwanza,
Amina Kisero alisema kuwa sheria ya ndoa
ya mwaka 1971, imeelza kuwa umri wa kuolewa kwa msichana ni miaka 14 au 15 wakati kanuni ya adhabu siura ya sita
sheria za Tanzania namba 1 na 2(i)
kinaahalalisha kitendo cha ubakaji kwa kigezo cha kuolewa.
“Vipengele vyote hivi ni kikwazo kwa mustakabali wa
ulinzi wa haki za mtoto , na haki ya afya
ya uzazi kwa mujibu wa sheria ya mtoto
ya mwaka 2009, tunataka kama katiba mpya itatambua na kuweka bayana juu ya
ulinzi wa mtoto wa kike sheria hizi zitafungwa” a;lisema Kisero
Kwa upande wake Khadija Haddy ambaye pia ni mtaalam wa afya
ya Jamii kutoka YAP alisema kuwa mtoto
wa kike mwenye umri wa chini ya miaka 18
maumbile yake hayana uwezo wa kupokea mabadiliko ya kubeba ujauzito na
kuzaa kwa wakati unaotakiwa.
Alisema kuwa ndo za utotoni zinasababisha tatizo kubwa la
kuongezeka kwa magonjwa ya wanawake kutokana na maumbile yao kushindwa kubeba
mabadiliko ya kimwili.
Kwa mujibu wa takwimu ya UNFPA za mwaka 2013 tatizo la ndo za utotoni
linakuwa kwa kasi nchini licha ya kampeni kubwa ya wananchi inayopigwa
kupambana na hali hiyo. Wilaya ya Shinyanga ikiongoza kwa asilimia 59, Tabora
asilimia 58,Mara asilimia 55, Dodoma asilimia 51 na lindi asilimia 45.
Kongamano hili linaandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba
kwa kushirikiana na TGNP Mtandao mjini Dodoma na kuwashirikisha wanawake na
wanaume na makundi yote ya kijamii zaidi
ya 200 na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.
Mwisho
No comments:
Post a Comment