Friday, September 12, 2014

UWASILISHWAJI WA MAPENDEKEZO YA KAMATI BUNGE MAALUM LA KATIBA KIKAO CHA 35



Katika mchakato wa uwasilishwaji wa mirejesho ya mapendekezo ya kamati juu ya rasimu ya pili ya katiba, kulingana na mijadala iliyofanyika kwenye kamati. Leo ilikuwa ni sura ya 11 na 15 zinazohusu Utumishi wa Umma katika Jamuhuri ya Muungano  na ulinzi na usalama wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mfuatano. Katika uwasilishwaji wajumbe walijikita zaidi katika sura hizo na kuja na mapendekezo kama ifuatavyo;
Katika kutetea haki na usawa wa kijinsia katika utumishi wa umma, kamati zilizo nyingi zimependdekeza kuwa usawa wa kijinsia utambulike kuwa moja juu ya ajira na uteuzi wa Viongozi wa taasisi katika serikali kutambua usawa wa kijinsia. Hivyo basi katika ibara ya 185 (1) iongezwe fasili inayo beba dhana ya usawa wa kijinsia katika uteuzi wa viongozi na wa taasisi za kiserikali ili kufikia malengo kama taifa ya 50/50 katiaka nafasi za utumishi wa umma.
Pia katika ibara ya 186(3)inayotoa sifa za Mwenyekiti na Wajumbe katika Tume ya Utumishi wa Umma, katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma itakayo undwa na Rais, fasili inayotambua uzingatiaji wa usawa wa kijinsia iongezwe na kuwa fasili (e) katika ibara hii . hii ni kutokana sifa pendekezwa hazitoi fursa sawa kwa jinsia na usawa wa uwakilishi wa jinsia.
Katika sura ya 15 inayozungumzia Ulinzi na Usalama wa Jamuhuri ya Muungano, kamati zimependekeza mambo yafuatayo ili kuhakikikisha nchi inakuwa yenye usalama na amani kwa mali, rasilimali na raia wake.
Kamati karibu zote zimependekeza ibara ya 235(2) kwa madai kuwa hakijitoshelezi na kimefanyiwa marekebisho Kwa kuongeza “mito” “maziwa” na “maliasili” hivyo kusomeka kama ifuatavyo; “Usalama wa Jamuhuri ya Muuunganao unahusu ulinzi wa miapaka yote ya eneo la Jamuhuri ya Muuungano ikiwa ni pamoja na ardh, maliasili, anga, mito, maziwa na bahari kuu, watu wake, mali zao, haki uhuru na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje ya nchi”. Hili ni jambo jembe kwa ulinzi na usalama wa maliasili, usalama , haki na mali za raia wake kwa ustawi wa taifa lenye amani na maendeleo kwa wote bila uonevu na unyonyaji usiokuwa na tija katika taifa.
Katika ibara ya 236 inayohusu vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa, kamati zimetoa mapendekezo ya kutamka wazi kuatambulika kwa idara ya Uhamiaji kiakatiba kama moja ya chombo cha ulinzi na usalama wa Taifa. Hicyo basi ibara hii ya imependekezwa kuongezwa fasili (d) inayo sema “Idara ya Uhamiaji” pia iwekwe fasili inayoelekeza juu ya nafasi ya uteuzi wa Kamishina mkuu wa Uhamiaji kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Kuanzishwa kwa Baraza la ulinzi na Usalama wa Taifa, mapendekezo ya kamati zote zimependekeza juu ibara ya 237 kuwa iongezwe fasili inyomtambua Rais kama mjumbe na mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa. Kutokama na umuhumu wake kama Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wan nchi, bila kufanya hivyo itaiweka nchi katika hatari ya kuweza kuvuruga amani.
Katika uteuzi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, rasimu ya kataba haijasema wazi juu ya usawa wa jinsia kwani pia wanawake wanstahiri kuteuliwa katika nafasi nyeti na muhimu kama ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama. Mapendekezo yote ya kamati hakuna hata moja iliyosema kuwa jinsia izinagatiwe katika taasisi hizi za serikali bali walijikita zaidi katika uwianao sawa wa pande mbili za muuungano. Ibaraya 240,245 na 249 ziko kimya kabisa juu ya haki hii ya msingi kwa wanawake katika idara hizi. Pia kuna changamoto kubwa sana pia kuwa idara ya Magereza imesahaulika kabisa; haijatajwa kwa kuzingatia ni taasisi muhimu sana katika maswala ya ulinzi na usalama wa raia katika Taifa letu.
pia, kuwekewa masharti kwa taasisi , kampuni na vyombo binafsi vya ulinzi na usalama viwekewe masharti kikatiba. Fasili hii itasidia kuvitambulisha na Bunge kupewa mamlaka ya kutunga sheria itakayo vithibiti na pia kuweka mfumo wa undwaji na utekelezaji wa majukumu yake.
Hitimisho, katika mawsilisho ya leo usawa wa kijinsia umengumziwa sana lakini si katika usawa saw wa uwakilishi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Hili ni jambo muhimu sana na aina yake kutiliwa mkazo ili kuhakikisha katika taasisi zote usawa wa kijinsia unazingatiwa.




No comments: