MTANDAO
WA JINSIA TANZANIA - (TGNP)
GDSS
10/09/2014
MADA;
Uwasilishwaji taarifa za kamati Bunge Maalum la Katiba; Je, Masuala ya Kijinsia
yamezingatiwa?
Mtoa
Mada: TGNP Mtandao na Timu ya ufuatiliaji na uchambuzi (MAT)
Mchakato wa kutafuta
katiba mpya unaendelea mjini Dodoma kwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba
katika kuwasilisha mapendekezo ya mijadala yao kutoka kwenye kamati zao. Kamati
zote 12 zimepata fursa ya kuwasilisha maoni ya waliowengi na hata wachache
ambao kwa namna moja ama nyingine walishindwa kukubaliana katika baadhi ya
mambo.
Kulingana na
uwasilishwaji wa taarifa za kamati zimeibuka hoja nyingi zenye kuleta
mustakabali mzuri kama taaifa. Licha ya hoja tata kama muundo wa serikali ya
muungano, na mambo mengine yenye msisimko wa kipekee kwenye rasimu ya katiba
pendekezwa na Tume ya kukusanya maoni iliyoongozwa na Jaji Joseph Sinde
Walioba.
Katika mchakato wa katiba
moja ya madai ya msingi kabisa ni usawa wa kijinsia kikatiba, wananchi
wanapendekeza katiba yenye mrengo wa kijinsia (Gender Sensitive Constitution).
Lakini itapendeza tukikumbushana dhana ya usawa wa kijinsia kabla ya kujadili
hoja iliyo mbele yetu juu ya katiba na masuala ya kijinsia. Usawa wa kijinsia “ni hali ya mwanamke na mwanaume kuwa na fursa sawa na upatikanaji wa
haki zenye kuleta tija, katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ya Jamii, kati ya
makundi haya mawili”.
Kwa nini usawa wa
kijinsia uwepo katika katiba mpya?
Katiba ni sheria mama
inayolinda haki za raia wote (wanawake na wanaume na watoto) nchini, na
kuhakikisha mfumo wa kuendesha nchi na wajibu wa viongozi wanaopewa dhamana ya
kuongoza. Hivyo ni muhimu sheria hii mama iwe imebeba masuala au haki za
makundi haya mablimbali nchini kwa kudumisha maendeleo yenye tija.
Wote tunatambua jitihada
za TGNP na asasi nyingine za kiraia kwa
kuwa mstari wa mbele kuhakikisha katiba ya wananchi inapatikana yenye kubeba
msingi kuu wenye mrengo wa kijinsia. TGNP kwa kushirikiana na Mtandao wa
wanawake ana Katiba (WFT) Ilitoa mapendekezo ya msingi kabisa yanayotakiwa
kuingizwa kwenye rasimu na klatiba mpya ili kuleta msingi wa usawa wa kijinsia
katika nyanja zote. Kulingana na mapendekezo hayo na mchakato wa katiba mpya
unaoendelea, napenda sasa tujadili kwa pamoja;
je uwasilishwaji huu wa mapendekezo umezingatia masuala ya kijinsia?
Kulingana na
mawasilisho yote ya sura zilizoweza kuwasilishwa baadhi ya mambo yamejitokeza
katika ibara mbalimbali pia maeneo mengine yako kimya kabisa kama ifuatavyo;
Haki ya mtoto ibara ya
43(2), wajumbe wamependekeza iweke tafsili rasmi ya nani ni mtoto? Kwa
kuzingatia zaidi haki za mtoto wa kike, ulinzi na usalama wake. Wajumbe walio
wengi wamependekeza tafsili ya mtoto iwekwe bayana kikatiba. Isomeke wazi -
mamlaka ya nchi itaweka utaratibu wa sheria utakaowezesha utekelezaji na
usimamizi wa haki za mtoto, hususani mtoto wa kike.
Pia, Ibara ya 44
inayotambulisha haki na wajibu wa kijana katika shughuli za maendeleo.
Mapendekezo ya wachache yameonyesha kwa kiasi kikubwa jinsi ibara hii ilivyo
jumla jumla, aidhi kukosekana kwa dhana inayonyambua na kuonyesha jinsi zote
mbili. Hivyo kamati zimeshindwa kutoa pendekezo msingi itakayobainisha haki na
wajibu wa kijana katiaka kujiletea maendeleo. Bila kusahau pendekezo muhimu
litakalo tambua “vijana kufaidi fursa na haki sawa; kuwa na usawa katika kufikia na
kumuliki rasilimali na usawa katika ulinzi”.
Vile vile, haki ya mtu
mwenye mlemavu, limezungumzwa Kwa uzito wake ikiwemo haki ya kutobaguliwa,
kupata huduma za Jamii Kama wengine, kulindwa juu ya vitendo vya unyanyasaji,
ukatili na kuabaguliwa. Lakini haki ya mwanamke mweleulemavu zimepewa nguvu
sana na walemavu wenyewe na si wajumbe kutoka makundi mengine. Hivyo basi wabunge
wote bila kujali nakundi yao inatakiwa kwa pamoja kutetea haki za walemavu
kikatiba has haki za wanawake walemavu kikatiba.
Suala
la Katiba kutambua usawa wa jinsia
katika umiliki wa rasilimali na kutumia. Ibara mpya inayounda Tume ya taifa
ya ardhi itakayo hakikisha misingi na falsafa ya umiliki wa ardhi inazingatia
usawa wa kijinsia katika matumizi ya ardhi imependekezwa na kamati zilizo
nyingi. Suala hili ni zuri kwasababu limeweka bayana dhamira ya katiba kufikia
usawa wa kijinsia kwa kumpa mwanamke fursa ya kutumia rasilimali. Ibara hii
ikipitishwa itampa mwanamke fursa ya kujitegemea kiuchumi kwa kutumia ardhi. Hata
hivyo, tunaona kwamba ibara hii haijafafanua mbinu au utaratibu utakaotumika na Tume
katika kuzingatia usawa na nafasi ya mwanamke katika mgawanyo wa hizo
rasilimali. Pia, ibara hii itamke bayana kwamba wanawake wanahaki ya
kumiliki ardhi isiyo hamishika, ikiwemo ardhi ya ukoo na haki ya kurithi.
Itambulike kuwa, takribani 5% tu ya wanawake wanafanya kazi ya kilimo ya ardhi
chini ya miliki yao, 44% ya wanawake wanafanya kazi ya kilimo katika ardhi
inayo milikiwa na waume zao na 35% ya wanawake wanafanya kazi katika ardhi
inayomilikiwa na ukoo. (chanzo:
Dailynews.co.tz/index/php/feature/24296-tanzania).
Wajumbe wamependekeza iundwe tume ambayo itakua kituo kikuu cha
serikali itakayoratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu usawa wa jinsia na
maendeleo ya jinsia.Tume hii itapewa nguvu kusimamia masuala ya upangaji wa
jinsia katika mipango yote ya Taifa. Imependekezwa ibara namba 214 iongezewe
kipengele (a)Itakayosomeka,kutakua na tume ya jinsia itakayoongozwa na
mwenyekiti na makamu mwenyekiti na
wajumbe wasiopungua watano; 2. Majukumu yatakua ni pamoja na kuendeleza,
kulinda na kutetea haki na usawa jinsia na kutoa taarifa yake bungeni angalau
mara moja kwa mwaka. Na mwisho bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji
wa ibara hii.
Hata
hivyo wajumbe waliwasilisha mapendekezo kuhusu usajili wa Vyama vya siasa kwamba ili chama cha siasa kiweze kusajiliwa
lazima kioneshe suala la usawa wa kijinsia katika taratibu za uendeshwaji wake.
Katika sura ya 12(a) ibara ya 197 inayozungumzia juu ya usajili wa vyama vya
siasa pia kusisitiza katiaka uteuzi wa masajili wa vyama vya siasa uzingatie
usawa wa kijinsia ili kutekeleza usawa katika uongozi unaozingatia jinsia zote
sawa.
Wajumbe
pia, walitoa mapendekezo kuhusu kuwa na Tume huru na ya haki ya Uchaguzi kwa
kupendekeza kwamba uteuzi wake uzingatie usawa wa kijinsia na walemavu kutoka
pande mbili za Jamuhuri ya muungano, ibara ya 190 na 191 na fasili zake
zote. Wamependekeza iwepo ibara maalum inayotamka bayana juu ya uteuzi
unaozingatia swala hili. Pia mapendekezo yamezingatiwa wajumbe ambao watajiliwa
kusimamamia tume ya uchaguzi wasiwe wanajihusisha na chama chochote cha siasa
ili kuepusha ukosefu wa haki na usawa wakati wa uchaguzi.
Katika kutetea haki na
usawa wa kijinsia katika utumishi wa umma, kamati zilizo nyingi zimepedekeza
kuwa usawa wa kijinsia utambulike kuwa moja juu ya ajira na uteuzi wa Viongozi
wa taasisi katika serikali kutambua usawa wa kijinsia. Hivyo basi katika ibara ya 185 (1) iongezwe fasili inayo beba
dhana ya usawa wa kijinsia katika uteuzi wa viongozi na wa taasisi za
kiserikali ili kufikia malengo kama taifa ya 50/50 katika nafasi za utumishi wa
umma.
Pia katika ibara ya 186(3)inayotoa sifa za Mwenyekiti na
Wajumbe katika Tume ya Utumishi wa Umma, katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya
Utumishi wa Umma itakayo undwa na Rais, fasili inayotambua uzingatiaji wa usawa
wa kijinsia iongezwe na kuwa fasili (e) katika ibara hii . hii ni kutokana
sifa pendekezwa hazitoi fursa sawa kwa jinsia na usawa wa uwakilishi wa jinsia.
Katika
uteuzi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, rasimu ya katiba
haijasema wazi juu ya usawa wa jinsia kwani pia wanawake wanstahiri kuteuliwa
katika nafasi nyeti na muhimu kama ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Mapendekezo yote ya kamati hakuna hata moja iliyosema kuwa jinsia izinagatiwe
katika taasisi hizi za serikali bali walijikita zaidi katika uwianao sawa wa
pande mbili za muuungano. Ibara ya 240,245 na 249 ziko kimya kabisa juu ya haki
hii ya msingi kwa wanawake katika idara hizi. Pia kuna changamoto kubwa sana
pia kuwa idara ya Magereza imesahaulika kabisa; haijatajwa kwa kuzingatia ni
taasisi muhimu sana katika maswala ya ulinzi na usalama wa raia katika Taifa
letu.
Huduma
bora ya afya ibara ya 47(1) rasimu haukunyumbua vilivyo fasili
hii iliyobeba uhai na usalama wa wananchi juu ya mazingira bora kiafya. Wajumbe
wamepndekeza kifungu hiki kiongezewa uzito kwa kutamka wazi haki ya uzazi
salama,kupata huduma bora ya afya kutambulika kikatiba. Katiba itunge fasili
inayolipa Bunge nguvu ya kutunga sheria
itakayoweka msingi muhimu ya haki ya uzazi salama kwa kuhakikisha huduma hizi zinatolewa
bure, zenye ubora na usalama wa miindombinu ambayo ni rafiki pia kuwalinda
wajawazito na kazi ngumu ambazo zinaweza hatarisha usalama wa afya ya mama na
mtoto aliyetumboni. Vilevile kuzingatiwa kwa uzazi salama kwa walemavu, lugha
za kibaguzi, mazingira rafiki kimiundombninu inawafanya wakati mwingine kupata
rapsha zisizokuwa na sababu katika hali nguvu waliyokuwa nayo.
Kwa kiasi fulani,
masuala ya kijinsia yamezingatiwa kwenye uwasilishaji na kutiliwa mkazo wakati
wa majadiliano ya mjumbe mmoja mmoja yanayoendelea. Kuna changamoto bado katika
kuyazungumzia maswala haya kwa kutetea haki na usawa wa kijinsia, maswala hayo
hayajazungumzwa kwa undani unaotakiwa ukilinganisha na mapendekezo yaliyotolewa
na asasi mbalimbali zinazotetea haki za wanawake ikiwepo Jukwaa la Wanawake na
katiba kwa mfano uundwaji wa chombo cha kitaifa kitakacho ratibu masuala yote
yahusuyo jinsia ambayo itakuwa mkombozi na mtetezi wa masuala ya kijinsia
ikisaidiwa na asasi za kiraia na mashirika yanayotatea kimataifa. Kulingana na
mwenendo wa Bunge bado inahitajika kuendelea kusisitizia kwa mkazo mambo haya
na kumpa mwanamke heshima anayo stahili.haya ni baadhi ya masuala machache tuu
kati ya yale yaliyogusiwa, pia yapo
mengi hayakuguswa juu haki na usawa wa kijinsia.
Hali
kadhalika uwasilishwaji wa ibara ya 98
imesahau kabisa haki sawa ya uteuzi licha ya swala la ubunge na uwaziri, ibara
hii ibainishe misingi ya haki kijinsia katiba uteuzi wa nafasi hizo na
kuleta uwiano wa kijinsia (50/50%) katika nafasi hizo.
Katika suala la Uteuzi wa majaji, kamati nyingi zimeshindwa kuonyesha
jinsi usawa wa kijinsia ulivyo zingatiwa. Tungependa kuona usawa wa asilimia
hamsini kwa hamsini katika uteuzi wa majaji.
No comments:
Post a Comment