Na Mwandishi Wetu
Kuna hofu
kubwa miongoni mwa wanawake kuwa hoja ya usawa wa kijinsia wa 50/50 katika
nafasi za maamuzi iliyoaninishwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba mpya inaweza kuondolewa kutokana na wajumbe wa wabunge la Katiba kutokuielewa.
Akizungumza kwenye Kongamano
la wanawake kutoka mikoa yote nchini
Tanzania lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwa kushirikiana na
TGNP Mtandao mjini Dodoma Mwenyekiti wa Mfuko wa Wanawake Profesa Ruth Meena
amesema kuwa baada ya kukutana na
wajumbe was Bunge maalum la Katiba na kujadiliana juu ya kuendelea kuzingatia masuala
ya kijinsia katika mijadala inayoendelea kuanzia kesho Jumanne amesema
wamebaini kuwa kuna masuala muhimu ya usawa wa kijinsia ambayo yameachwa.
“Tumefuatilia na kuwasikiliza,
tumegundua kuwa wenyewe (wajumbe) hawaelewi maana halisi ya usawa wa kijinsia
na dhana ya 50 kwa 50 ambayo imeainishwa kwenye rasimu. Hii inapaswa kuwa
agenda muhimu sana ya kufuatilia katika kipindi hiki”alisema Prof. Ruth
Meena amesema kuwa mchakato umeanza kwa kukusanya maoni yao
na kuwa na mambo ambayo yatawaunganisha wote. Mchakato huo uliibua mambo mengi
haswa katika mabaraza ya Katiba. Mwanzo kabisa masuala ya wanawake yalikuwa 12,
tunapaswa kuendelea kudai yasitupwe yote”alisema Profesa Ruth.
Profesa Meena amesema
kuwa kila siku wanawake 24 wanafariki wakijifungua, hivyo Mtandao wa wanawake
na katiba wamesema kwamba kujifungua kusiwe ni hukumu la kifo.
Pia amesema kuwa ni lazima 50 kwa 50 katika uongozi
izingatiwe.
Mjumbe wa Bunge maalum la
katiba kwa tiketi ya taasisi ya elimu Dk.
Avemaria Semakafu, amesema kuwa yeye na wenzake walioko bungeni watahakikisha
wanapigania agenda ya mwanamke kuwa na haki sawa kama mwananchi yoyote na kamwe
hawatayumbishwa na agenda za wanasiasa.
Mshiriki Anna Kiombo kutoka
Mbeya alisema kuwa ni lazima haki za
wanawa na kuheshimiwa katika katiba mpya.
“Ni lazima jamii ielewe kuwa
hakuna maendeleo ya taifa lolote bila kuwa na katiba inayozingatia uasawa wa
kijinsia na haki za wanawake kutambulika, wanawake wa vijijini tunateseka na
kunyanyasika kwabsabu hatutambuliki kwenye katiba mpya”alisema.
Leo jumanne umati huo wa
wanawake utaendesha Bunge mbadala mjini hapa kwa lengo la kuyapa makundi yote
ya wanawake nafasi ya kueleza madai yao
kwenye Bunge halisi linaloendelea mjini Dodoma.
Akizungumza aliyekuwa
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Usu Mallya amesema kuwa wameamua kuendesha
Bunge mbadala mjini Dodoma ili kuamsha
uelewa na umakini kwa wananchi zaidi kuendelea kufuatilia mchakato, kutoa fursa kwa wananchi wengine kupaaza sauti zao nje ya Bunge maalum, kuonesha jinsi ambavyo wangependa Bunge hilo
liendeshwe.
Aidha Bunge mbadala litasaidia
kuonesha masuala ya kijinsia ambayo hayajazingatiwa kikamilifu na kudai
yaingizwe kwenye katiba kwa muda huu uliobaki.
Mashirika mengine ambayo
yanashiriki ni TAMWA, Oxfam, WILDAF,KIVULINI na mengine kutoka mikoa
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment