Friday, September 5, 2014

UCHAMBUZI WA HARAKA BUNGE LA KATIBA KIKAO CHA 32 SEPTEMBA 4, 2014



Katika bunge la 33 kamati zilijikita katika sura ya 9 na 10 zinazohusu Bunge la Jamuhuri ya Muungano na mahakama ya Jamuhuri ya Muungano.
Ibara ya 113(1) inayopendekeza  rais kutokuwa sehemu ya bunge na kupendekeza kamati nyingi zimependekeza mfumo uliokuwa unatumika katika katiba ya mwaka 1977 inayomtambua rais na wabunge kuwa ndio sehemu ya bunge. Kwa marekebisho haya msingi wa utawala bora utaondolewa kabisa kwa kufanya bunge kutokuwa huru. Tunapendaa kuwahasa wabunge wa bunge maalum la katiba kuheshimu ibara ya hiyo kama ilivyoainishwa kwenye rasimu ya pili ya katiba.
Hata hivyo, baadhi za kamati wamerekebisha ibara ya 128 na 129 kinacho wapa wananchi dhamana ya kuwawajibisha viongozi wao pale wanaposhindwa kuwawakilisha na kutetea maslahi yao, na kuwanyima wananchi dhamana hio. Tunakemea vikali kitendo hicho kwani kinawapa wabunge mwanya wakutumia vibaya cheo chao. Tunaona kwamba ibara inayowapa wananchi dhamana ya kumwajibisha wabunge wao kitawafanya wabunge wafanye kazi kwa bidii.
Hoja nyingine iliyokua imezungumziwa ni kuhusu kuzingatiwa kwa usawa wa jinsia  wakati wa uchaguzi wa spika na naibu spika. Baadhi za kamati zilipendekeza mfano; Spika wa jinsia ya kike akichaguliwa, basi naibu spika awe wa kiume na hivyo hivyo spika wa jinsia ya kiume akichaguliwa, naibu wake awe mwanake. Kulingana na rasimu ya katiba ibara ya (a) (135) iko kimya, hivyo basi baadhi ya kamati zinapendekeza kiongezwe kipengele katika ibara hii inayotambua sifa za mtu kuchaguliwa kuwa spika au naibu kwa kuzingatia usawa wa kijinsia ya 50/50 katika nafasi hii.
Katika uwasilishwaji wa mirejesho, baadhi ya kamati zimependekeza ibara ya 151(a) kinachsema maamuzi ya mahakama yatazingatia “kutenda haki kwa wote bila kuajli hali ya mtu kijamii, kisiasa,kiutamaduni au kiuchumi”, imependekezwa kuwa neno utamaduni liondolewe na kusomeka  “usawa wa kijinsia na makundi maalum”. Hili ni swala jema na la kupongezwa sana kwa uzingatiaji usawa na haki za kijinsia pia kujali haki na usawa kwa makundi yote.
Uteuzi wa majaji ndani ya mahakama ya juu, rufaa na za nchi washirika. Katika uwasilishwaji wa mapendekezo ya kamati, kamati uzingatiwaji wa jinsia katika uteuzi wa majaji wa mahakama. Kulingana na rasimu ya pili ya katiba kutozingatia haki kikatiba katika uteuzi wa majaji wa mahakama mchini. Ibara ya (c)(158)(3), 159 na 160 viko kimya juu ya uzingatiaji wa 50/50 na mirejesho ya kamati za bunge maalum la katiba imekaa kimya juu la swala muhimu kama hili. Japo Kuwa Tunapongeza Mapendekezo ya kushusha umri kuwa miaka 40, Tofauti na Ilivyo kwenye Ibara ya 158 (3) inavyosema miaka 45.
Haya, ni mambo muhimu yaliyojitokeza katika uwasilishaji ambayo timu yetu inayofuatilia mchakato wa  katiba na Bunge maalum imeona kwa jicho la haraka. Usikose kufuatilia zaidi uchambuzi wetu wa leo ambao tutauleta kwenu kesho asubuhi.

No comments: