Monday, October 6, 2008

Uchaguzi Tarime kuna walakini !!

Wanaharakati, Tarime ina dalili ya kuelekea kwenye machafuko kwa kutaka kutawala kwa nguvu zote.

Nahisi ni upigaji wa kura ndani ya mfumo wa kijeshi. Hii inaonyesha bila kutumia jeshi ushindi ni kitendawili.

Pia kunavitendawili vingi sana Tarime,kama majina ya wapiga kura kokosekana, msimamizi wa uchaguzi kudai
Atahakikisha watu wanapiga kura pamoja na kasoro zilizojitokeza kwenye majina yao, komputa kukosea????

Hivi kati ya komputa na mtumiaji wa komputa ni nani anayekosea?

Inabidi tulivalie njuga suala la tume huru ya uchaguzi kama tulivyo livalia suala la EPA na kaka zake.

Wanaharakati mnasemaje?

1 comment:

Anonymous said...

Ukweli ni kwamba tume ya uchaguzi ina matatizo mengi, inabidi wanaharakati tupiganie hili na tuandamane mpaka kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na ikiwezekana mpaka kwa Rais.

Major Majaliwa