Thursday, October 23, 2008

Kupanda Mlima Kilimanjaro kutetea Haki za Binadamu

Wanaharakati,

Naomba fursa kwenye blogu ya jamii kuwatangazia Wanaharakati na watu wengine wote kuwa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu [LHRC], kinaandaa maadhimisho ya miaka 60 ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu ambapo kilele chake kitakuwa Tarhe 10 Disemba 2008.

Katika kuelekea huko, Kituo kitakuwa na mambo kadhaa, ikiwemo kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia (kama wanachama wa WiLDAF) kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba, kuwa na jumuiko la wasaidizi wa kisheria (paralegal symposium), mkutano wa wasaidizi wa kisheria vijijini (village legal workers' meeting), wiki ya msaada wa kisheria (legal aid services) na mkutano w maadhimisho ya siku ya haki za Binadamu yenyewe tarehe 10 Disemba. Haya yatafanyika mjini Dodoma.

Pamoja na hayo, Kituo kinafanya mipango ya kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Tarehe 22 Novemba, pamoja na mambo mengine kupinga ukatili wa kijinsia na kupandisha Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights) pale Uhuru Peak ili unaofahamu na usiofahamu tamko hili ili kuweza kuangaza na kutetea haki za binadamu kutoka kwenye kilele kirefu kuliko vyote Afika.
Watu wote wanakaribishwa.

3 comments:

Anonymous said...

utetezi wa haki za binadamu liwe jambo linaloendelea duniani kote siku zote, kwani ukosefu wa hakki za binadamu katika eneo moja la dunia linasababisha kukosekana kwa haki katika eneo ambalo linaloonekana kama lina haki sana.

Anonymous said...

wanaharakati wazitumie siku hizo kumi na sita kukumbuka matatizo wanayokutana nayo wanawake katika jamii na wapange mbinu za kukutatua matatizo hayo hapo baadae. kila la kheri wanaharakti....

Anonymous said...

harakati hizi ni muhimu sana na ziendelee kila mwaka natumaini watu wanapata msg inayokusudiwa na wanaharakati. kazi njema. by eva