kaimu Mkurugenzi Mtendaji TGNP, Bi. Lilian Liundi akizungumza na wasanii kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es salaam |
usu Akiendelea |
Wasanii wakifuatilia mafunzo hayo kwa umakini mkubwa |
Wasanii waliofika wakiwa wametulia |
Wasanii walioshiriki wakiwa kwenye makundi kujadili zaidi baada ya mtoa mada kuwapa fursa ya kubunga bongo |
wasanii walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa wanahabari waliofika kwaajili ya coverage ya tukio hilo |
WASANII wametakia kutumia nafasi
wanazopata kupanda majukwaani kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na kudai
uwajibikaji na upatikanaji wa huduma za
kijamii .
Akizungumza na wasanii walioshiriki warsha ya siku moja ya TGNP
iliyolenga kuwajengea uwezo wasanii kutumia nafasi yao katika kudai
uwajibikaji, uandaaji wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia na mapambano dhidi ya
ukatili wa kijinsia jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP
Mtandao, Lilian Liundi amesema kuwa
wanasanii wana nafasi kubwa ya kutoa elimu, kuburudisha, kuonya na
kukemea na kuleta mabadiliko chanya.
Amewataka kutumia ipasavyo fursa
walio nayo kuhakikisha wanapata uelewa
wa masuala yanayowagusa wananchi na kuandaa kazi zitakazosaidia kuleta
mabadiliko, kama filamu, Michezo ya majukwaani, mashairi, ngoma, na uchoraji wa
vibonzo.
“TGNP Mtandao tunafanya kazi na
vyombo vya habari kwa muda mrefu, wasanii tunawatambua kama watoa taarifa pia,
na mtindo wao wa utoaji wa taarifa ni wa haraka na unapendwa na wengi, ndio
manaa tunakutana na wasanii kwaajili ya kuwawezesha kutumia fursa walizo nazo
kupaaza sauti juu ya changamoto za kijamii”alisema Liundi
Alisema kuwa kila msanii ana
hadhira yake na kama atakuwa na uelewa
juu ya masuala ya bajeti kwa mrengo wa kijinsia, akijua masuala muhimu
yanauyohusu mgawanyo sawa wa rasilimali hasa kwa makundi yaliyoko pembezoni,
akajengewa uwezo wa kufanya uchambuzi wa majukumu ya kijinsia na mahitaji
muhimu lazima jamii itabadilika na
watendaji au watunga sera nao watapata ujumbe na kuleta mabadiliko.
Kwa upande wake Mwanachama na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Usu Mallya, alisema
kuwa Utandawazi na soko huria ambavyo vimeingia kuanzia miaka
ya 1990 vimeipelekea serikali kupunguza wajibu wake wa kusimamia uchumi, ajira,
masoko na biashara, sekta binafsi imepewa majukumu makubwa zaidi ya kuwa injini
ya kutafuta biashara na masoko na kupelekea kuongezeka kwa tabaka na wanawake wamezsidi kubaki nyuma kiuchumi.
“ Tunahitaji sana nguvu ya
wasanii katika kuelimisha jamii na kushinikiza mabadiliko. Mwanamke kujitoa
kwenye umasikini ni kazi ngumu sana, pamoja na majukumu aliyo nayo lakini bado
hana maamuzi kuhusu fedha za kutekeleza majukumu aliyo nayo”alisema Usu
Kwa upande wake Stara Thomas,
mwimbaji wa siku nyingi alisema kuwa
katika semina hiyo amepata mamabo makubwa ikiwa ni pamoja na kuuelewa
mfumo dume ni kitu gani na jinsi unavyoadhiri maendeleo ya jamii hasa wanawake
na watoto.
“katika semina hii nimejifunza
kitu kikubwa, nimeelewa maana ya mfumo dume na jinsi unavyoadhiri jamii, nitatumia elimu hii katika kazi zangu za sanaa
ili kuleta mabadiliko”alisema Thomas
Naye Mwimbaji Irene Sanga,
alisema kuwa wasanii wanatakiwa kuitumia nafasi waliyo nayo kuandaa kazi
ambazo zitafikisha ujumbe wa kuleta mabadiliko sio mapenzi pekee. “sisi
tuna nguvu tunaweza kuleta mabadiliko,
bila wasanii hakuna sherehe wala misiba, tunauwezo mkubwa wa
kujibadilisha na kubeba uhusika wa kila aina tutumie vizuri fursa hizi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment