JUMUIYA ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa),
kimewataka wananchi kuweka siasa kando pale unapofika wakati wa kujadili
masuala yanayohusu mustakabali wa taifa.Pia, Udasa imesema iwapo
raslimali za taifa zitasimamiwa na kutumika vizuri kwa mapato
yanayopatikana, wananchi wake wataondokana na ugumu wa maisha.
Hayo
yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Udasa, Dk Francis Michael
alipokuwa akizungumzia Kongamano la kujadili Mstakabali wa Taifa kwa
miaka 50 ijayo ya uhuru, litakalofanyika chuoni hapo Desemba 9, mwaka
huu.
Dk Michael alisema kongamano hilo halilengi kukuza mitazamo
ya kisiasa, bali litakuwa na nia ya kulijenga taifa kwa vizazi vijavyo.
Alisema
mada kuu ‘Uhuru Wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 ijayo’,
Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala kufungwa na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
No comments:
Post a Comment