Shirika Huru la Habari (Tanpress)
limemtaka Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi
Nchini (IGP), Said Mwema na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk.
Emmanuel Nchimbi.
Limesema viongozi hao wanatakiwa kuwajibishwa kutokana na mauaji ya
mwaandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi
Mwangosi yaliyotokea mkoani Iringa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Tanpress,
Mobini Sarya, imeeleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael
Kamuhanda anatakiwa kuwajibika kutokana na amri yake aliyoitoa wakati wa
vurugu kati ya polisi na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleoi
(Chadema).
Shirika hilo limeitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
itoe ufafanuzi kwa kushindwa kutoa tamko na msaada kufuatia kifo cha
mwandishi huyo licha ya kwamba polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji
hayo.
“Kuna mauaji ya watu watano yaliyotokea Tarime ambayo yalifanywa na polisi walitoa ubani kwa familia zao.”
Shirika hilo limeziomba nchi wafadhili zinazotoa misaada kuhusu ukuaji
wa demokrasia na utawala bora ziangalie kama ina umuhimu kwa sasa
kutokana na nchi wanayoifadhili kutoheshimu utawala bora.
No comments:
Post a Comment