|
Wawezeshaji kutoka TGNP weakijadiliana na wasimamizi wa MAISHA PLUS hapo kijijini kabla ya kuanza kufundisha |
|
wanakijiji wa MAISHA PLUS wakiwa tayari wamekaa wakisubiri kupata darasa kutoka TGNP |
|
Wawezeshaji kutoka TGNP Deo Temba na Agnes Lukanga wakikaribishwa na 'Babu' wa MAISHA PLUS kijijini |
|
"babu" akisisitiza jambo kuhusu darasa la TGNP kijijini |
|
Babu ni lazima achekeshe na kuingiza utani kwenye utambulisho |
|
Deo temba kutoka TGNP akiwezesha kijijini hapo |
|
Mshiriki wa MAISHA PLUS kutoka Uganda akichangia hasa kueleza uingizaji wa masuala ya kijinsia kwenye mchanakto wa kuandaa bajeti za kitaifa |
|
Mwezeshaji Agness Lukanga akiwezesha |
|
Mshiriki wa MAISHA PLUS kutoka Burundi akichangia |
|
Mshiriki wa MAMA SHUJAA kijijini akichangia |
|
Wanawake wanashiriki kama walezi wa vijana na wakijifunza zaidi masuala ya kilimo na wanawake |
|
washiriki wakiwa na wawezeshaji wakiwa na bango la TGNP linaloonesha mzigo anaoubeba mwanamke kutokana na kutokuwa na bajeti yenye jicho la kijinsia na mchango wake kutokutambuliwa. bango hilo liliibua mdajala mpana na washiriki wote kutoka nchi za Afrika ya mashariki walisema tatizo lipo nchi zote |
Na TGNP Staff
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), imepata fursa ya kuwawezesha na kuwanjengea
uwezo washiriki wa programu ya Maisha Plus na mama shujaa inayofanyika kila
mwaka mara moja.
Katika uwezeshaji huo ambao
uliwezeshwa na wafanyakazi wa TGNP
Mtandao uliwawezesha washiriki hao
kuibua mijadala kuhusu ushiriki wa jamii
katika kuandaa bajeti ya mrengo wa Kijinsia na ushiriki wa wananchi wa
pembezobi katika kaundaa bajeti na ibebe masuala ya wananchi hasa wanawake.
Pilika pilika zilionekana katika
kijiji cha Maisha Plus ambapo wanakijiji walionekana wakishughulisha na
shughuli binafsi za kifamilia, kubadilishana mawazo na uzoefu walionao. Pia
waliweza kupata darasa kutoka kwa wawezeshaji kutoka TGNP Mtandao.
Lengo la darasa hili ni kuwawezesha washiriki
wa Maisha Plus vijana na mama shujaa wa chakula kutambua na kuelewa masuala ya
kijinsia kwenye shughuli zao za kazi wanazozifanya kwani washiriki wanatoka sehemu
mbalimbali na wanajishughulisha na kazi tafauti ambazo zinatofautiana wengine
ni wasanii, waandishi wa habari, wafanyakazi wa taasisi mbalimbali, wengine
bado ni wanafunzi wanaendelea na masoma.
Tunajua kwamba wakipata masuala
muhimu ya kutetea usawa wa kijinsia na wanayaelewa huko wanapofanya kazi zao
baadaye watayatumia vizuri sana na wataweza kuleta mabadiliko katika nchi yetu
ndiyo maana tumeshiriki kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunawajengea uwezo kwenye
kampeni ya ‘Haki ya Kiuchumi: Rasilimali
Ziwanufaishe Wanawake Walioko Pembezoni’ alisema Deogratius Temba, Afisa
Habari wa TGNP Mtandao.
Aliendelea na kusema kuwa
tumefurahi sana kuwepo na mjadala huu mpana kupitia picha chokozi na kuona ni
fursa pekee kuendelea kusambaza kampeni ya Haki
ya Uchumi kwa jamii nzima mjini na huko vijijini kwasababu watu walio
vijijini ni wengi na watakapoenda kule
wataendeleza hii kampeni na lubadilisha jamii yetu ya kitanzania.
Suala la na mfumo dume na umiliki
wa ardhi limejitokeza wakatii wa majadiliano kwani mfumo dume na umiliki wa
uchumi vinashirikiana kwamba kama kuna mfumo dume mwanamke na kijana hawawezi
kumiliki uchumi hivyo kuendelea kubeba
mzigo mkuwa wa kulea familia.
Wanakijiji wa Maisha Plus
walifurahishwa na mjadala huu kwani una nia ya kumkomboa mwanamke kutokana na
yale majukumu mazito anayokuwanayo nyumbani na jamii nzima inayomzunguka na
kuwa na haki ya kumiliki ardhi na siyo kuwa mzalishaji pekee kama ilivyo sasa
katika jamii nyingi hapa nchini. Vile vile wameweza kuona umuhimu wa kuhudhuria
vikao vya kijiji ambapo wanaweza kupata fursa ya kutoa maoni na kushiriki moja
kwa moja katika mchakato wa bajeti ya serikali kupitia serikali ya mtaa ambapo
wengi wao hawakuwa na ufahamu huo.
Mama shujaa pia walitoa uzoefu
wao kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii wanazotoka na kusema kuwa umiliki wa
ardhi kwa kinamama bado ni changamoto kwani wengi wao wamebaki kuwa wazalishaji
tu na kutumia ile ardhi na siyo kumiliki jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi
za kinamama katika kujikomboa kiuchumi. Vile vile walipongeza waandaaji kwa
kuwa na mpango wa kutoa mafunzo mbalimbali yatakayowasaidia washiriki katika
sehemu walizotoka na jamii kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment