Tuesday, June 3, 2014

TGNP MTANDAO YAMPOTEZA MWANACHAMA MWANZILISHI NA MWENYEKITI WA KWANZA



TGNP Mtandao
TANZIA
TGNP MTANDAO YAMPOTEZA MWANACHAMA MWANZILISHI NA MWENYEKITI WA KWANZA
                 DADA FIDES SIWANGU CHALE              







  

1940 - 2014
TGNP Mtandao tumepata pigo kubwa  kwa kumpoteza mwanaharakati na Mwenyekiti wa kwanza wa shirika, aliyefariki Juni 2, 2014 Ubungo Msewe Dar es Salaam.
Fides Chale alikuwa ni mwalimu na kiongozi aliyegusa maisha ya wengi hapa Tanzania, Mwanaharakati mtetezi wa haki za wanawake, wasichana na makundi mengine yaliyoko pembezoni.
Dada Fides amekuwa mtu wa watu, mcheshi, mwenye upendo, utu, huruma, mpole, mwenye sura ya kutabasamu muda wote hata alipokuwa kwenye hali ya ugonjwa.
Tunapoombeleza kumpoteza dada yetu Fides Chale, tunasheherekea maisha yake  mchango wake mkubwa jinsi alivyojitolea kwa hali na mali kulilea shirika tangu lilipoanza  hadi mauti yalipomfika. Fides Chale  alishika uongozi  TGNP wakati shirika likiwa changa, kuliwekea misingi imara na endelevu wa kiuongozi, kiutawala, na  mfumo mzuri wa kubadilishana uongozi unaoendelea hadi leo.
Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani Ubungo Msewe. Alhamis 05/06/2014 ibada itafanyika katika Kanisa Katoliki Mt. Petro  Osterbay na kufuatiwa na mazishi katika makaburi ya Kinondoni.
Imetolewa na
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
TGNP Mtandao

No comments: