Friday, July 18, 2008

Mrejesho wa Mada Juu ya Kilimo Cha Bio Fuel Tanzania.

Mada hii ilijadiliwa tarehe 16/07/2008 na iliweza kuibua changamoto nyingi ambazo zinahitajika kufanyiwa kazi. Mada iliwakilishwa na Mtendaji Mkuu wa HakiArdhi, Bw. Myenzi na Bw William Olenasha kutoka Shirika la Oxfarm. Wawakilishaji walitoa mada kulingana na utafiti uliofanywa na mashirika yao katika maeneo ambayo tayari makampuni yapatayo 37 yameonesha nia ya kutaka ardhi na baadhi yamekwishapata ardhi katika maeneo hayo. Maeneo ambayo wawekezaji wameonekana kuweka msisitizo ni pamoja na; Lindi, Mtwara, Morogoro, Iringa, Tanga, Kigoma, Rukwa na Mara. Hadi sasa makampuni 16 yameomba na kupewa ardhi inayofikia hekta 641, 170 na ekari 1150. Kwa wastani yapo maombi ya ardhi kuanzia ekari 30,000 hadi 2,000,000, na makampuni hayo yamewekeza wastani wa dola 60 million hadi 1.5 bilioni.

Baadhi ya faida ambazo zinasemekana zinaweza kutokana na uwekezaji huo wa kilimo cha mazao ya biofuel ni pamoja na; fursa za ajira, fursa za masoko kwa bidhaa na mazao, upatikanaji wa nishati vijijini na mijini, kukua kwa uchumi wa wananchi, kupungua kwa umasikini, na kupungua kwa wimbi la nguvu kazi kukimbilia mijini.

Wahusika wakubwa wa miradi hii ya bio-fuel ni makampuni kutoka nchi za Sweeden, Uholonzi, Ujerumani, Uingereza, Ubelgiji, Australia, na Afrika Kusini. Makampuni mengine yamefikia hatua ya kufika vijijini na kuwashawishi wananchi hadi kupata ardhi ni pamoja na; Biofuels la Uingereza, awali waliomba hekta 20,000 katika vijiji vya wilaya ya Kisarawe na hadi mwisho wakapewa hekta 9,000. Kwa wilaya ya Bagamoyo wapo SEKAB kutoka Sweeden, wao walihitaji hekta 500,000 mpaka mwisho walipewa hekta 50,000 na mchakato wa kutafuta ardhi zaidi bado unaendelea.

Nchi kama Brazil ambayo inayotolewa mfano kama nchi iliyofaidika na kilimo cha bio-fuel, inatumia zaidi ya 85% ya ethanol yote inayozalishwa nchini humo. Sekta hiyo inaajiri kati ya watu laki saba hadi milioni moja, wengi wao ni vibarua tu na ujira wao ni mdogo sana na katika mazingira magumu ya kazi. Idadi ya ajira hizo imekuwa ikishuka kila siku kutokana na uvunaji wa kutumia mashine. Tayari mashine imeshachukua 40% ya nafasi za ajira na mwaka 2010 itachukua 70% na kuna sheria kuwa ifikapo 2017 uvunaji utakuwa kwa mashine tu. Swali la kujiuliza vipi hapa kwetu Tanzania?

Mapungufu Makubwa katika uwekezaji wa kilimo hiki cha bio-fuel hapa Tanzania ni pamoja na;
• Hakuna sera hadi sasa wala sheria au kanuni juu ya kilimo cha bio-fuel.
• NBTF ndio imeundwa tangu 2006 iko katika mchakato wa kutengeneza mwongozo (Guidelines) ambazo hazielewiki zitakuwa na hadhi gani, ya sheria au la?
• Wawekezji wanakwenda moja kwa moja kwa wanakijiji wasio na uelewa wa maswala ya ardhi hivyo uwezekano wa kuwarubuni ni mkubwa
• Uelewa wa jamii juu ya maswala haya bado uko chini kwani wengi wanavutwa na ahadi za haraka bila kujali athari za muda mrefu.

Athari tarajiwa kutokana na uwekezaji huu ni pamoja na;
• Uhaba wa ardhi ya kilimo kwa mazao ya kilimo.
• Bei za vyakula kuendelea kupanda zaidi.
• Kuendelea kwa hali duni ya tabaka la wanyonge hasa wanawake wa vijijini kwa sababu wao ndio wazalishaji wakubwa wa chakula cha familia.

Wanaharakati walipendekeza yafuatayo yafanyike:
• Zoezi zima la wawekezaji kuwinda ardhi vijijini lisitishwe hadi sera na sheria zitakapotungwa na kujadiliwa na wananchi kwa mapana wakizingatia tija na athari za bio-fuel.
• Elimu itolewe zaidi kwa umma juu ya bio-fuel.
• Wananchi wakatae kuondolewa kwa nguvu katika maeneo yao bila mjadala mrefu juu ya fidia kwa viwango vya soko badala ya kupangiwa viwango na mwekezaji.
• Uwekezaji mkubwa uelekezwe katika nishati mbadala zinazotokana na jua, upepo, na maporomoko ya maji.

Muda wa kushauriana sana umekwisha juu ya swala hili, wanaharakati wanapaswa kuchua hatua za haraka kuzuia uporaji huu wa ardhi ya Watanzania kwa kivuli cha uwekezaji. Nani yupo tayari kuwa mstari wa mbele kutetea ardhi ya Watanzania?

12 comments:

Anonymous said...

kilimo ndio uti wa mgongo nchini kwetu Tanzania ni lazima tukipe kipao mbele bila hatutaweza kupiga hatua

Nuru Luksasi

upendo group

Anonymous said...

kwanza hatufahamu maana halisi ya kilimo cha Bio Fuel kwa hiyo tungepata uelewa kwanza halafu ndio tungeweza kuchangia mada hii kwa uraisi
Mwansiti Omary
upendo group

Anonymous said...

Tunahitaji nguvu ya pamoja kukuhakikisha arhi ya watanzania inarudishwa na si hivyo tu hata elimu kwa wanakijiji haswa na watanzania kupia vyombo vya habari na mikutano ya wanakijiji.

Anonymous said...

mimi nadhani serikali ingetazama huu ukoloni mpya unatka kuja tena katika nchi yetu la sivyo kizazi kijacho kitakuja kutulaumu sisi kwa kushindwa kutetea ardhi yetu inayoporwa.
mwanaharakati.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

acheni ujinga bwana, nyie vp? kwanza mnaotoa comments andikeni majina yenu, mnaogopa nini nyie si ni wanaharakati?
harafu na we blog admn, acha kuogopa kuweka commetrs zetu hapa hata kama comments zenyewe zinawakasirisha wazungu. najua tgnp kuna wazungu wanaonufaika lakini ukweli lazima usemwe kwani kawaida ya ukweli ni kuuma hata km haukwepeki. sema tulisema nini haya mambo ya kuangalia uppande mmoja acheni vinginevyo funga hii blog kama mnaanza kuwatetemekea mabosi wenu ok!

Anonymous said...

mimi naona biofuel inaharibu mazingira ya nchi yetu tuachane na kilimo cha namna hii.
mimi zainabu msangi hekima group

Anonymous said...

mambo yanatisha kweli hapa nchini, unaweza kutamani kufa,sawa tutalima mafuta je viwanda tunavyo vya kufua hayo mafuta? na je wataalamu tunao kwa sasa!

Anonymous said...

hi mambo zenu, tunahaja kubwa ya kuuelimisha umma wa tz hasa kule kijijini kwetu maana hata haya mambo hawayafahamu kabisa hata hiyo bio fuel hawaijui, wao wakiambiwa watakubali tu wakidhani ndio mkombozi wao. hivi haya masuala tumeyatafakari kwa kina? au tunakurupuka tu! je tumejiandaa vya kutosha? tukahamasishe kwa kutumia ngoma za asili tutaelewana vizuri. kamala hatuogopi kuandika majina bali tuanpitiwa tu, si unajua mashikolo mageni. hariet wa kabende, makuburi wda ugali mwema.

Anonymous said...

ardhi ni mali ya watanzania wote ni nani huyo anaeruhusu biofuel bila hata kutuuliza sisi vijana. wavunje magorofa huko kwao waanzishe kilimo biofuel. hatutaki kuibiwa ardhi mwisho wataturudisha katika umasikini.
mimi mwanafunzi shaghufta msangi.

Anonymous said...

je hicho kilimo cha biofuel mimi kama mtanzania nitafaidika vipi.ninawasiwasikwambahiyondio njia ya kutumaliza sisi wanyonge na ardhiniyetu safina husseni msuya. shirikisho msanii afrika.

Anonymous said...

je?mimi kama mwanafunzininafaidikavipi na kilimo chabiofuel ninawasiwasi hiyondiyo njia yakutuujumu naardhiniyetu. jamillah joseph

Anonymous said...

Great work.