SEMINA ZA JINSIA
DEMOKRASIA NA MAENDELEO (GDSS) 25/09/2013 ILIYOFANYIKA VIWANJA VYA TGNP MTANDAO
MADA: Tathmini ya Tamasha la Jinsia 2013
MWEZESHAJI: Mary
Nsemwa kutoka TGNP
WASHIRIKI: 66 (39 Ke/27 Me)
Mchakato:
Mwezeshaji aliwapitisha washiriki kwenye malengo makuu ya
Tamasha la Jinsia 2013, na kisha kuwapitisha kwenye kazi za Kamati mbali mbali
zilizokuwa zimeundwa zifanye kazi kabla na wakati wa Tamasha, ili kuhakikisha
malengo ya Tamasha yanafikiwa.
Kisha, washiriki waligawanyika kwenye vikundi vinne kujadili
Kamati nne tofauti kwa kuangalia mambo yafuatayo:
·
Mafanikio
makubwa matatu kwa Kamati husika
·
Maeneo
ya kuboresha na njia mahsusi tatu za kuboresha
·
Ushiriki
wa wana GDSS kwenye Tamasha lijalo uboreshwe vipi.
Kamati za Tamasha la
Jinsia 2013 zilizofanyiwa uchambuzi ni:
·
Kamati
Kuu
·
Kamati
ya Utafutaji Rasilimali na Utawala
·
Kamati
ya Ushiriki
·
Kamati
ya Habari, Taarifa na Mawasiliano
Kwa ujumla wa Kamati
zote nne zilizojadiliwa, mambo yafuatayo yalijitokeza kutoka kwenye vikundi
hivi vinne kama mafanikio:
·
Kwa kuingiza Bunge la
Wananchi na Mahakama ya Wazi; maudhui ya Tamasha la mwaka huu yalikuwa tofauti yenye ubunifu
uliohamasisha ushiriki wa hali ya juu
tofauti na miaka mingine;
·
Watoa
mada za msingi (plenary) walikuwa mahiri, na warsha zilitumia mbinu shirikishi
(uraghbishi) zilizofanya ushiriki kuwa mkubwa na mpana.
·
Washiriki
wote kupatiwa chakula ilisaidia kutulia
na bila kupoteza muda kwenda
kutafuta chakula.
·
Washiriki
wote kushiriki kikamilifu na kuchangia mijadala
·
Vikundi
vya sanaa vilifanya sanaa zenye
maudhui yanayoendana na mada na kuibua mjadala mkubwa.
·
Tamasha
lilifanikiwa kutangazwa sana kwenye redio, televisheni, mitandao ya kijamii,
magazetini n.k. kabla, wakati na baada ya Tamasha
Maeneo yafuatayo
yalitajwa kuhitaji maboresho kwenye matamasha yajayo:
·
Idadi
ya warsha ipunguzwe maana inaleta mkanganyiko kwa washiriki na zinapungua
ufanisi
·
Muda
wa majadiliano ya plenary na kwenye warsha uongezwe
·
Huduma
ya chakula iboreshwe; na washiriki
wapakuliwe chakula cha kutosha na maji ya kunywa yatolewe wakati wa chakula
·
Wana
GDSS wajulishwe mapema kutokuwepo kwa uwezeshwaji wa nauli ili wajiandae
·
Taarifa
za Tamasha zitolewe na kusambazwa miezi mitatu au zaidi kabla
·
Gharama
za mauzo ya vikoi, tshirt, begi n.k. zijulikane mapema ili washiriki wajipange
mapema kununua.
Ushiriki wa wana GDSS kwenye Tamasha
lijalo uboreshwe vipi?:
·
Ratiba
itoe nafasi zaidi kwa vikundi vya GDSS kushiriki kuto mada na kuonesha sanaa zao
·
Fursa
za kujitolea (volunteers) zichukue wana GDSS w wengi zaidi
·
Kazi
za maandalizi ya Tamasha kama vile usafi, kupaka rangi, useremala, mama lishe
n.k. zitangazwe mapema ili wana GDSS wajipange na kuomba kuzifanya.
Makubaliano kuelekea Tamasha la Jinsia
2015:
·
Kuwe
na maandalizi ya mapema kwa wana
GDSS hususan semina maalum kwa wana GDSS
kabla ya Tamasha ili waelewe vizuri mada kuu ya Tamasha, warsha zitakazokuwepo
n.k ili ushiriki wao uwe na ufanisi zaidi
·
Tamasha
la mwaka 2015, litakuwa mwaka wa Uchaguzi Mkuu Tanzania na huenda tukawa na
Katiba mpya tayari, tutumie fursa hizi kuhakikisha linafana zaidi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment