|
Mwanachama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania
(TGNP) Bi. Asseny Muro akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya
katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatano, Jan. 9,
2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni
Mwenyekiti wa TGNP Bi. Mary Rusimbi na Mjumbe wa Bodi ya mtandao huo
Prof. Ruth Meena. |
|
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba Jaji Joseph Warioba akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya
leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam. Kulia kwa Jaji Warioba ni Bi. Ussu Mallya, Mkurugenzi Mtendaji
wa mtandao huo, Prof. Ruth Meena 9Mjumbe wa Bodi ya TGNP) na Mwenyekiti
wa TGNP Bi. Mary Rusimbi. |
|
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Dkt. Sengondo Mvungi akiongea katika mkutano na Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP) uliolenga kupata maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya
leo (Jumatano, Jan. 9, 2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Wajumbe wengine wa Tume Bi. Mary Kashonda na
Bi. Salma Moulidi. |
|
TGNP pamoja na Tume Ya Mabadiliko ya Katiba katika Picha ya Pamoja |
|
Mwananchama wa Mtandao wa Jinsia Tanzania
(TGNP) Bi. Subira Kibiga akitoa maoni ya mtandao huo kuhusu Katiba Mpya
katika mkutano na Tume ya Mabadiliko ya Katiba leo (Jumatano, Jan. 9,
2013), katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam. Wengine ni wananchama
wenzake Bi. Diana Mwiru (kushoto) na Bi. Asseny Muro. |
Na Deogratius Temba
MTANDAO wa Jinsia Tanzania
(TGNP), leo wamekutana na Tume ya Kuratibu mchakato wa Katiba Mpya katika ofisi
za Tume hiyo zilizoko jijini Dar es salaam.
TGNP waliongozwa na Mkurugenzi
Mtendaji Usu Mallya, Mwenyekiti wa Bodi Mary Rusimbi naMkuu wa Taasisi ya Mafunzo
ya Jinsia, wakuu wa idara, wanachama,
wafanyakazi na wawakilishi wa vikundi
vya kijamii vinavyoshiriki katika shughuli za harakati na TGNP.
Wakizungumza wakati wa
kuwasilisha maoni yao kwa mtazamo wa Kijinsia, wanaharakati hao wamesema kuwa
katiba mpya ni lazima itambue mchango wa wanawake katika maendeleo na uchumi wa
taifa haswa kutambua shughuli za wanawake sizizo na kipato au sizizo rasmi.
Haki za wanawake na usawa wa kijinsia katika mgawanyo wa rasilimali na nafasi
za kutoa maamuzi serikali, haki za msingi za kijamii kama maji, afya, elimu,
kilimo na ufugaji.
TGNP wameshauri Tume
kuhakikisha inachukua masuala ya msingi yanayohusu wanajamii walioko pembezoni
hasa wanawake na kuyaingiza kwenye katiba mpya ili changamoto ambazo zimekuwa
zikimkabali Mwanamke ziondoke kabisa au kupungua baada ya kupatikana kwa katiba
mpya.
Kwa upande wake Mjumbe wa Tume
Mary Kashonda, alisema kuwa wanaharakati
kutoka TGNP wana nafasi kubwa katika kuhakikisha wanatoa maoni yanayobeba sauti
za wanawake walioko pembezoni hata wasio jua kusoma kutokana na ukaribu wao na
jamii hasa wanawake wa pembezoni.
“Wanawake
wengi huko vijijini hawawezi kuzungumza mbele ya wanaume, na ukiwaambia
waandike hawawezi kwasababu hawajui kusoma na kuandika. Hili ni tatizo, Nyie
TGNP mna fursa ya kukutana nao na kuwasilikiza
wakizungumza maoni yao ni muhimu sana…. Bila shaka mnayo”alisema
Kashonda.
No comments:
Post a Comment