Friday, September 12, 2014

UWASILISHWAJI WA MAPENDEKEZO YA KAMATI BUNGE MAALUM LA KATIBA KIKAO CHA 35



Katika mchakato wa uwasilishwaji wa mirejesho ya mapendekezo ya kamati juu ya rasimu ya pili ya katiba, kulingana na mijadala iliyofanyika kwenye kamati. Leo ilikuwa ni sura ya 11 na 15 zinazohusu Utumishi wa Umma katika Jamuhuri ya Muungano  na ulinzi na usalama wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mfuatano. Katika uwasilishwaji wajumbe walijikita zaidi katika sura hizo na kuja na mapendekezo kama ifuatavyo;
Katika kutetea haki na usawa wa kijinsia katika utumishi wa umma, kamati zilizo nyingi zimependdekeza kuwa usawa wa kijinsia utambulike kuwa moja juu ya ajira na uteuzi wa Viongozi wa taasisi katika serikali kutambua usawa wa kijinsia. Hivyo basi katika ibara ya 185 (1) iongezwe fasili inayo beba dhana ya usawa wa kijinsia katika uteuzi wa viongozi na wa taasisi za kiserikali ili kufikia malengo kama taifa ya 50/50 katiaka nafasi za utumishi wa umma.
Pia katika ibara ya 186(3)inayotoa sifa za Mwenyekiti na Wajumbe katika Tume ya Utumishi wa Umma, katika uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma itakayo undwa na Rais, fasili inayotambua uzingatiaji wa usawa wa kijinsia iongezwe na kuwa fasili (e) katika ibara hii . hii ni kutokana sifa pendekezwa hazitoi fursa sawa kwa jinsia na usawa wa uwakilishi wa jinsia.
Katika sura ya 15 inayozungumzia Ulinzi na Usalama wa Jamuhuri ya Muungano, kamati zimependekeza mambo yafuatayo ili kuhakikikisha nchi inakuwa yenye usalama na amani kwa mali, rasilimali na raia wake.
Kamati karibu zote zimependekeza ibara ya 235(2) kwa madai kuwa hakijitoshelezi na kimefanyiwa marekebisho Kwa kuongeza “mito” “maziwa” na “maliasili” hivyo kusomeka kama ifuatavyo; “Usalama wa Jamuhuri ya Muuunganao unahusu ulinzi wa miapaka yote ya eneo la Jamuhuri ya Muuungano ikiwa ni pamoja na ardh, maliasili, anga, mito, maziwa na bahari kuu, watu wake, mali zao, haki uhuru na maslahi mengine ya kitaifa dhidi ya vitisho vya ndani na nje ya nchi”. Hili ni jambo jembe kwa ulinzi na usalama wa maliasili, usalama , haki na mali za raia wake kwa ustawi wa taifa lenye amani na maendeleo kwa wote bila uonevu na unyonyaji usiokuwa na tija katika taifa.
Katika ibara ya 236 inayohusu vyombo vya ulinzi na usalama wa Taifa, kamati zimetoa mapendekezo ya kutamka wazi kuatambulika kwa idara ya Uhamiaji kiakatiba kama moja ya chombo cha ulinzi na usalama wa Taifa. Hicyo basi ibara hii ya imependekezwa kuongezwa fasili (d) inayo sema “Idara ya Uhamiaji” pia iwekwe fasili inayoelekeza juu ya nafasi ya uteuzi wa Kamishina mkuu wa Uhamiaji kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.
Kuanzishwa kwa Baraza la ulinzi na Usalama wa Taifa, mapendekezo ya kamati zote zimependekeza juu ibara ya 237 kuwa iongezwe fasili inyomtambua Rais kama mjumbe na mwenyekiti wa Baraza la Ulinzi na Usalama wa Taifa. Kutokama na umuhumu wake kama Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wan nchi, bila kufanya hivyo itaiweka nchi katika hatari ya kuweza kuvuruga amani.
Katika uteuzi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, rasimu ya kataba haijasema wazi juu ya usawa wa jinsia kwani pia wanawake wanstahiri kuteuliwa katika nafasi nyeti na muhimu kama ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama. Mapendekezo yote ya kamati hakuna hata moja iliyosema kuwa jinsia izinagatiwe katika taasisi hizi za serikali bali walijikita zaidi katika uwianao sawa wa pande mbili za muuungano. Ibaraya 240,245 na 249 ziko kimya kabisa juu ya haki hii ya msingi kwa wanawake katika idara hizi. Pia kuna changamoto kubwa sana pia kuwa idara ya Magereza imesahaulika kabisa; haijatajwa kwa kuzingatia ni taasisi muhimu sana katika maswala ya ulinzi na usalama wa raia katika Taifa letu.
pia, kuwekewa masharti kwa taasisi , kampuni na vyombo binafsi vya ulinzi na usalama viwekewe masharti kikatiba. Fasili hii itasidia kuvitambulisha na Bunge kupewa mamlaka ya kutunga sheria itakayo vithibiti na pia kuweka mfumo wa undwaji na utekelezaji wa majukumu yake.
Hitimisho, katika mawsilisho ya leo usawa wa kijinsia umengumziwa sana lakini si katika usawa saw wa uwakilishi kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Hili ni jambo muhimu sana na aina yake kutiliwa mkazo ili kuhakikisha katika taasisi zote usawa wa kijinsia unazingatiwa.




Friday, September 5, 2014

UCHAMBUZI WA HARAKA BUNGE LA KATIBA KIKAO CHA 32 SEPTEMBA 4, 2014



Katika bunge la 33 kamati zilijikita katika sura ya 9 na 10 zinazohusu Bunge la Jamuhuri ya Muungano na mahakama ya Jamuhuri ya Muungano.
Ibara ya 113(1) inayopendekeza  rais kutokuwa sehemu ya bunge na kupendekeza kamati nyingi zimependekeza mfumo uliokuwa unatumika katika katiba ya mwaka 1977 inayomtambua rais na wabunge kuwa ndio sehemu ya bunge. Kwa marekebisho haya msingi wa utawala bora utaondolewa kabisa kwa kufanya bunge kutokuwa huru. Tunapendaa kuwahasa wabunge wa bunge maalum la katiba kuheshimu ibara ya hiyo kama ilivyoainishwa kwenye rasimu ya pili ya katiba.
Hata hivyo, baadhi za kamati wamerekebisha ibara ya 128 na 129 kinacho wapa wananchi dhamana ya kuwawajibisha viongozi wao pale wanaposhindwa kuwawakilisha na kutetea maslahi yao, na kuwanyima wananchi dhamana hio. Tunakemea vikali kitendo hicho kwani kinawapa wabunge mwanya wakutumia vibaya cheo chao. Tunaona kwamba ibara inayowapa wananchi dhamana ya kumwajibisha wabunge wao kitawafanya wabunge wafanye kazi kwa bidii.
Hoja nyingine iliyokua imezungumziwa ni kuhusu kuzingatiwa kwa usawa wa jinsia  wakati wa uchaguzi wa spika na naibu spika. Baadhi za kamati zilipendekeza mfano; Spika wa jinsia ya kike akichaguliwa, basi naibu spika awe wa kiume na hivyo hivyo spika wa jinsia ya kiume akichaguliwa, naibu wake awe mwanake. Kulingana na rasimu ya katiba ibara ya (a) (135) iko kimya, hivyo basi baadhi ya kamati zinapendekeza kiongezwe kipengele katika ibara hii inayotambua sifa za mtu kuchaguliwa kuwa spika au naibu kwa kuzingatia usawa wa kijinsia ya 50/50 katika nafasi hii.
Katika uwasilishwaji wa mirejesho, baadhi ya kamati zimependekeza ibara ya 151(a) kinachsema maamuzi ya mahakama yatazingatia “kutenda haki kwa wote bila kuajli hali ya mtu kijamii, kisiasa,kiutamaduni au kiuchumi”, imependekezwa kuwa neno utamaduni liondolewe na kusomeka  “usawa wa kijinsia na makundi maalum”. Hili ni swala jema na la kupongezwa sana kwa uzingatiaji usawa na haki za kijinsia pia kujali haki na usawa kwa makundi yote.
Uteuzi wa majaji ndani ya mahakama ya juu, rufaa na za nchi washirika. Katika uwasilishwaji wa mapendekezo ya kamati, kamati uzingatiwaji wa jinsia katika uteuzi wa majaji wa mahakama. Kulingana na rasimu ya pili ya katiba kutozingatia haki kikatiba katika uteuzi wa majaji wa mahakama mchini. Ibara ya (c)(158)(3), 159 na 160 viko kimya juu ya uzingatiaji wa 50/50 na mirejesho ya kamati za bunge maalum la katiba imekaa kimya juu la swala muhimu kama hili. Japo Kuwa Tunapongeza Mapendekezo ya kushusha umri kuwa miaka 40, Tofauti na Ilivyo kwenye Ibara ya 158 (3) inavyosema miaka 45.
Haya, ni mambo muhimu yaliyojitokeza katika uwasilishaji ambayo timu yetu inayofuatilia mchakato wa  katiba na Bunge maalum imeona kwa jicho la haraka. Usikose kufuatilia zaidi uchambuzi wetu wa leo ambao tutauleta kwenu kesho asubuhi.

Thursday, September 4, 2014

TGNP Mtandao wakiendesha Bunge Mbadala (Bunge Kivuli) Dodoma

Washiriki kutoka kundi la walemavu wakiozungumza

Mshiriki kutoka kundi la walemavu wasiosikia akizungumza

Mwanaharakati Salome Nyoti akizungumza  kama mwongozaji

Wanaharakati vijana kutoka DSM wakitoa ngonjera yao kwa hisia kali

Maandamano ya wanaharakati mjini Dodoma kudai mauala yao iangizngiwzwe kwenye katiba

Maandamano yakiendelea

Maandamano yakiendelea

Vijana wakitoa ujumbe mzito kwa njia ya sanaa

Mwenyekiti wa Bunge Mbadala (Kivuli) akiongoza maandamano

Washiriki wakiingia








Bunge maalum la katiba Mbadala (Kivuli)m likiendelea


TGNP Mtandao na Mtandao wa wanawake na katiba waendesha mdahalo Dodoma

Wanawake kutoka jamii ya kifugaji wakizungumza

mshiriki kutoka Manyara akizungumza

Mshiriki kutoka bagamayo akizungumza

washiriki wakiendelea

Mwanachama wa TGNP na mwanaharakati wa masuala ya Jinsia Gemma Akilimali akizungumza

Mwanachama wa TGNP na mwanaharakati kutoka Mwanza, Maimuna kanyamala akizungumza

Umri wa ndoa uwe miaka 18- 21 -wanaharakati


Watu wanaoishi na changamoto za ulemavu wakifuatilia mjadala huo Dodoma


Baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakifuatilia

Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba wakisikiliza madai ya wananchi kwenye rasimu ya Katiba itakayojadiliwa Bungeni wiki hii

Uongozi wa Bungwe Maalum la Katiba mbadala (Bunge Kivuli) wakiendelea kuongoza Bunge hilo Mjini Ddodoma, Katikati ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Dk. Visencia Shule

Mmoja wa wasichana mwenye miaka 14 akipiga magoti kuonesha huruma kwa wanaanchi na wajumbe wa Bunge maalum la katiba kuwa wasikubali kuendelea kuruhusu wasichana wadogo kuolewa. wasichana hao walitoa tamko lao kulaani kitendo cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuendelea kutumika hadi leo inayoruhusu wasichana wenye umri wa miaka 14 kuolewa

kundi la wasichana kutoka mikoa mbalimbali wakiomba katiba mpya ikataze ndoa za utotoni

WANAHARAKATI wanaoshiriki kongamano la Katiba  la kujadili masuala ya kijinsia yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye mjadala wa Bunge maalum la Katiba wamewataka wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kuhakikisha katiba mpya itakayotengenezwa inatamka  umri wa  kuolewa au kuoa uwe miaka 18 hadi 21 ili kuwapa nafasi watoto wa kike kupata nafasi ya kusoma na kukua.
Wakizungumza wakati wakiendesha Bunge kivuli au Bunge maalum maalum la Katiba lililoandaliwa na TGNP Mtandao kwa kushirkiana na Mtandao wa Wanawake na katiba  mjini Dodoma,  wanaharakati hao wamesema kuwa  wajumbe wa Bunge maalum bila kujali tofauti zao za kijinsi wanapaswa kuhakikisha wanapigania haki ya mtoto wa kike kuwa salama na kutokuolewa kabla ya kukomaa akiwa na umri wa chini ya miaka 18.
Akizungumza Mwenyekiti wa Bunge maalum Mbadala la Katiba Dk. Vicensia Shule amesema kuwa  wananchi wote wanatakiwa kuunganisha nguvu wakati huu wa mchakato wa Bunge la Katiba kuhakikisha masuala muhimu ya wanawake nay ale ambayo yanatoa ulinzi kwa makundi yaliyoko pembezoni yanazingatiwa na kuingizwa kwenye katiba mpya.
“hakuna taifa ambalo ni tajiri au watu wake wameendelea bila kupata elimu,   na kuzingatia usawa wa kijinsia. Haya yote yatafanyika kama kuna elimu ya kutosha kwa wasichana na kama wataolewa  wakiwa watoto hawataweza kupata elimu”alisema Dk Shule.
Mshiriki kutoka shirika la Active Youth of Tanzania Mwanza, Amina Kisero alisema kuwa  sheria ya ndoa ya mwaka 1971, imeelza kuwa umri wa kuolewa kwa msichana ni miaka  14 au 15 wakati kanuni ya adhabu  siura ya sita  sheria za Tanzania namba 1 na 2(i)  kinaahalalisha kitendo cha ubakaji kwa kigezo cha kuolewa.
“Vipengele vyote hivi ni kikwazo kwa mustakabali wa ulinzi  wa haki za mtoto , na haki ya afya ya uzazi kwa mujibu wa sheria  ya mtoto ya mwaka 2009, tunataka kama katiba mpya itatambua na kuweka bayana juu ya ulinzi wa mtoto wa kike sheria hizi zitafungwa” a;lisema Kisero
Kwa upande wake Khadija Haddy ambaye pia ni mtaalam wa afya ya Jamii kutoka YAP alisema kuwa  mtoto wa kike mwenye umri wa chini ya miaka 18  maumbile yake hayana uwezo wa kupokea mabadiliko ya kubeba ujauzito na kuzaa  kwa wakati unaotakiwa.
Alisema kuwa ndo za utotoni zinasababisha tatizo kubwa la kuongezeka kwa magonjwa ya wanawake kutokana na maumbile yao kushindwa kubeba mabadiliko ya kimwili.
Kwa mujibu wa takwimu ya UNFPA  za mwaka 2013 tatizo la ndo za utotoni linakuwa kwa kasi nchini licha ya kampeni kubwa ya wananchi inayopigwa kupambana na hali hiyo. Wilaya ya Shinyanga ikiongoza kwa asilimia 59, Tabora asilimia 58,Mara asilimia 55, Dodoma asilimia 51 na lindi asilimia 45.
Kongamano hili linaandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwa kushirikiana na TGNP Mtandao mjini Dodoma na kuwashirikisha wanawake na wanaume na makundi yote  ya kijamii zaidi ya 200 na wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.
Mwisho

Sunday, August 31, 2014

Uwakilishi 50/50 Bungeni: Wasiwasi watanda kwa wanawake




Na Mwandishi Wetu
Kuna hofu kubwa miongoni mwa wanawake kuwa hoja ya usawa wa kijinsia wa 50/50 katika nafasi za maamuzi iliyoaninishwa kwenye rasimu ya pili ya Katiba mpya  inaweza kuondolewa kutokana na wajumbe wa  wabunge  la Katiba kutokuielewa.
Akizungumza kwenye Kongamano la  wanawake kutoka mikoa yote nchini Tanzania lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba kwa kushirikiana na TGNP Mtandao mjini Dodoma Mwenyekiti wa Mfuko wa Wanawake Profesa Ruth Meena amesema kuwa  baada ya kukutana na wajumbe was Bunge maalum la Katiba na kujadiliana juu ya kuendelea kuzingatia masuala ya kijinsia katika mijadala inayoendelea kuanzia kesho Jumanne amesema wamebaini kuwa kuna masuala muhimu ya usawa wa kijinsia ambayo yameachwa.
“Tumefuatilia na kuwasikiliza, tumegundua kuwa wenyewe (wajumbe) hawaelewi maana halisi ya usawa wa kijinsia na dhana ya 50 kwa 50 ambayo imeainishwa kwenye rasimu. Hii inapaswa kuwa agenda muhimu sana ya kufuatilia katika kipindi hiki”alisema Prof. Ruth
Meena amesema kuwa mchakato umeanza kwa kukusanya maoni yao na kuwa na mambo ambayo yatawaunganisha wote. Mchakato huo uliibua mambo mengi haswa katika mabaraza ya Katiba. Mwanzo kabisa masuala ya wanawake yalikuwa 12, tunapaswa kuendelea kudai yasitupwe yote”alisema Profesa Ruth.

 Profesa Meena amesema kuwa kila siku wanawake 24 wanafariki wakijifungua, hivyo Mtandao wa wanawake na katiba wamesema kwamba kujifungua kusiwe ni hukumu la kifo.

Pia amesema kuwa ni lazima 50 kwa 50 katika uongozi izingatiwe.
Mjumbe wa Bunge maalum la katiba kwa tiketi ya taasisi ya elimu Dk.  Avemaria Semakafu, amesema kuwa yeye na wenzake walioko bungeni watahakikisha wanapigania agenda ya mwanamke kuwa na haki sawa kama mwananchi yoyote na kamwe hawatayumbishwa na agenda za wanasiasa.
Mshiriki Anna Kiombo kutoka Mbeya alisema kuwa  ni lazima haki za wanawa na kuheshimiwa katika katiba mpya.
“Ni lazima jamii ielewe kuwa hakuna maendeleo ya taifa lolote bila kuwa na katiba inayozingatia uasawa wa kijinsia na haki za wanawake kutambulika, wanawake wa vijijini tunateseka na kunyanyasika kwabsabu hatutambuliki kwenye katiba mpya”alisema.
Leo jumanne umati huo wa wanawake utaendesha Bunge mbadala mjini hapa kwa lengo la kuyapa makundi yote ya wanawake nafasi  ya kueleza madai yao kwenye Bunge halisi linaloendelea mjini Dodoma.
Akizungumza aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Usu Mallya amesema kuwa wameamua kuendesha Bunge mbadala mjini Dodoma ili kuamsha  uelewa na umakini kwa wananchi zaidi kuendelea kufuatilia mchakato,  kutoa fursa kwa wananchi wengine  kupaaza sauti zao  nje ya Bunge maalum,  kuonesha jinsi ambavyo wangependa Bunge hilo liendeshwe.
Aidha Bunge mbadala litasaidia kuonesha masuala ya kijinsia ambayo hayajazingatiwa kikamilifu na kudai yaingizwe kwenye katiba kwa muda huu uliobaki.
Mashirika mengine ambayo yanashiriki ni TAMWA, Oxfam, WILDAF,KIVULINI na mengine kutoka mikoa mbalimbali.